Chama cha soka nchini Croatia (HNS), kimesitisha mkataba na kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Niko Kovac baada ya kuona ameshindwa kufikia lengo la kuipelekea The Blazers kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.

Maamuzi ya viongozi wa shirikisho la soka nchini humo yalifikiwa baada ya matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Azerbaijan usiku wa kuamkia jana huku kumbukumbu ya kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Norway ikiendelea kutawala tangu mwishoni mwa juma lililopita.

Rais wa chama soka nchini Croatia, Davor Suker amesema ilikua vigumu kwake pamoja na wajumbe wengine wanaounda kamati ya juu ya uongozi kuvumilia matokeo mabovu yanayoendelea kujitokeza huku harakati za kucheza fainali za barani Ulaya zikififia.

Amesema ndani ya siku 10 watafanya maamuzi ya kumtangaza kocha mpya ambaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha anawavusha kutoka hapa walipo na kuelekea mbele ambapo huenda wakafanikisha namna yoyote ambayo itawasaidia.

Hata hivyo Suker amekataa kutaja ni akina nani ambao wanawania nafasi ya kurithi mikoba ya Niko Kovac, huku baadhi ya vyombo vya habari vikiendelea kutaja jina la meneja wa klabu ya Lokomotiva Zagreb, Ante Cacic kwa kuamini huenda akatangazwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Croatia.

Kovac, ataendelea kukumbukwa kwa juhdi zake za kuiwezesha Croatia kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, baada ya kuchukua nafasi ya Igor Stimac, mwezi Oktoba mwaka 2013.

Balotelli Awapiga Dogo La Kiaina Liverpool
Petit: Mpaka Leo Ninajutia Kusajiliwa Na Chelsea