Samia Suluhu Hassan amesema alitaka kusikia kauli ya Mwanasiasa Zitto Kabwe juu ya ufunguzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo Mkoani Kigoma, na kwamba uhalisia amemkabidhi kwa wananchi akimaanisha kuwa mambo ni safi.

Rais Samia ameyasema hayo, wakati akihitimisha ziara yake Mkoani hii leo Oktoba 18, 2022 alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika.

Amesema, “Nilitaka nimsikie Zitto atasema nini, lakini si mmeona kasema mwenyewe kuwa amenikabidhi kwenu wananchi, akiwa na maana ya kuwa mambo ni safi, mara ya mwisho wakati nakuja Kigoma nilikuta panasinzia, pamekosa maendeleo lakini leo ni tofauti.”

Rais Samia ameongeza kuwa, “nimekuja hapa nimefungua majengo mapya ya chuo Cha Ualimu cha Kibanga kilichopo kasulu Kigoma, pia nimeweka jiwe la msingi kuashiria ujengaji wa barabara ya Kabingo-Kibondo-Kasulu-Manyovu yenye km 260.6.”

“Lakini pia nimezima majenereta na kuzindua umeme wa Gridi ya Taifa kwa mkoa wa Kigoma, bila kusahau nimefungua ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma bila shaka sasa mambo ni shwari,” amesema Rais Samia.

Ujenzi shule za Wasichana kumkomboa mtoto wa kike
Waziri aishukuru Serikali ujenzi wa Hospitali