Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto kutoka Muhimbili, Zaituni Bokhari ameeleza maana ya jinsi tata, kuwa ni hali ya mtoto wa kike anazaliwa na kiungo za siri cha ndani kinakuwa kikubwa kuliko kawaida, ambacho mtu anashindwa kutambua kama ni uume au ni kiungo cha kike baada tu ya mtoto kuzaliwa.

Neno la kitaalamu ambalo hutumika kuelezea hali hiyo ya kushindwa kutambua kama mtoto ni wakike au wa kiume ni ‘Ambiguous Genitalia’.

“Lakini anakuwa na mashavu ya uke kama kawaida pamoja na matundu mengine muhimu kwenye uke wake, wakati mwingine unakuta yale mashavu yameungana ila kile kiungo cha siri cha ndani kinakuwa kidogo na kule chini unakuta kuna njia ya mkojo, ni maumbile yanayoleta utata” amefafanua Dkt.Bokhari.

Amesema kutokana na mkanganyiko huo wazazi wengi kutokuwa na uelewa wa kutosha, hushindwa kutambua mapema na hudhani ni hali ya kawaida.

“Unakuta mtoto analelewa kama vile wa kiume kumbe ni wakike au analelewa kama vile wa kike kumbe ni wakiume” amesema Dkt.Bokhari.

Mwanzoni mwa wiki hii kwa mara ya kwanza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na madaktari kutoka Saudia Arabia wamefanya upasuaji kwa watu waliokuwa na jinsi tata watatu.

Miongoni mwa waliofanyiwa ni kijana mmoja mwenye umri wa mika 16 ambaye awali alikuwa analelewa kwa jinsi ya kiume, lakini baada ya kumpima vipimo ikagundulika kuwa ni wakike na amefanyiwa upasuaji na sasa ataanza safari mpya ya maisha kuishi kama mtoto wa kike.

Mjamzito achomwa mshale tumboni, Kichanga chapona
Simbachawene alia na TV, Friji 'used' kuingia nchini