Jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikiongoza kwa kutekeleza, kunyanyasa na kutenda  na haswa kushindwa kuwapa misaada watoto wanapokuwa wanahitaji.

Kuangizia hili Balozi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na Muigizaji maarufu wa filamu  Tanzania Salma .S. Jabu ‘Nisha‘ kwa kushirikiana na viongozi wa nchi juni 26 ataungana na watoto mbalimbali wanaotokea mazingira magumu kwa ajili ya kufturu pamoja.

Katika ukumbi wa mikutano leo jijini Dar es Salaam uongozi wa nisha’s film productio pamoja na Muigizaji huyo wamesema kuwa futari hiyo itafanyika katika viwanja vya shule ya sekondari vya azania kuanzia saa 10:00 jioni mpaka saa 2:00 usiku.

_DSC1949

Pamoja na kuwepo kwa watoto wanaotoka mazingira magumu na wale waishio  mitaani naye Makamu wa rais Bi.Samia Suluhu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam na watu wengine maarufu wanatarajiwa kudhuria katika hafla hiyo.

Nisha amesema mpaka sasa tayari maandalizi yameshafanyika ya kutosha na utaratibu wa kuwafikia watoto  wote wanaoishi mbali na mji watapatiwa usafiri  huku akisisitiza ulinzi utakuwepo wa kutosha.

_DSC1972

Aidha Nisha ameiomba jamii kuitikia wito huu na kuwataka wale waishio kwenye vituo wawasiliane 0676 894246 au 0789586057 kwa ajiili ya kuweza kushiriki kwa Sadaka ambayo ameiandaa.

 

Sekta Zisizo rasimi Kunufaika na Huduma za Hifadhi ya Jamii
Louis van Gaal Afikiriwa AC Milan