Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Kawe ,Josephat Gwajima amesema kuwa ,endapo wanakawe watampatia nafasi ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atawezesha kuwepo kwa huduma ya gari la wagonjwa   kwenye kila kata .  

Gwajima ametoa kauli hiyo septemba 13 wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni eneo la Kawe na kuongeza kuwa atahakikisha maisha ya wanakawe yanaboreshwa .  

“Nikichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe nitaweka Ambulance kwenye kila Kata, watu wangu watakimbizwa hospitalini kwa haraka na jambo hili ni jepesi halihitaji Manispaa wala halihitaji Serikali”- amesema Gwajima .

Pia amesisitiza  kuwa yeye anauwezo mkubwa wa maarifa na hivyo hadanganyi na yupo kwenye  nafasi nzuri ya kutekeleza  kile ananchokisema.

 “Mwaka jana nilitembelea kule Marekani, ndiyo maana nakuawambia usifikiri unaongea na kilaza kwa taarifa yako mimi naongea Kijapan nimeandika vitabau vitano vya Kijapan ukienda Amazon unakuta vinauzwa,”.

Diego Simeone kuikosa Atletico Madrid kwa siku 14
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 14, 2020

Comments

comments