Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima, amefunguka kuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa klabu ya Yanga ajili ya kukamilisha usajili wake wakati wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16 mwaka huu.

Niyonzima amesema kuwa ni mapema mno kuweka wazi kuhusu kurudi kwake tena Yanga lakini siku si nyingi kila kitu kitakuwa hadharani na kufafanua kwamba mazungumzo yake na viongozi wa klabu hiyo yanaendelea vyema.

Aidha, Niyonzima ameongeza kuwa licha ya kwamba Yanga wamempandia ndege na kumfuata Kigali lakini pia kuna timu nyingine mbili kutoka Tanzania ambazo nazo yupo nazo kwenye mazungumzo baada ya kuonyesha nia ya kutaka saini yake.

“Kuna viongozi wawili wa Yanga nimekutana nao na tumezungumza, lakini sio hao tu kuna wengine kutoka kwenye klabu za Tanzania wamekuja na tumefanya mazungumzo, kwangu mimi ninachoangalia nani amekubali ninachotaka ili niweze kuitumikia klabu yake,” alisema

Niyonzima aliyetua Yanga mwaka 2012, pia aliitumikia Simba kwa misimu miwili kuanzia mwaka 2017
Kwa sasa anakipiga klabu ya AS Kigali ya Rwanda ambako ana mkataba wa miezi sita

Dimba

Bima ya mazao yawifikia wakulima nchini
Live: Kutunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa kwa Rais Magufuli, Mahafali ya 10 UDOM