Benchi la Ufundi la Mbeya Kwanza FC limetoa heshima kwa Ruvu Shooting kwa kusema ni timu yenye hadhi kubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo inawalazimu kuheshimu hilo wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa 14 utakaowakutanisha kesho Alhamis (Februari 03).

Ruvu Shootng itakua mwenyeji wa mchezo huo, huku ikiwa na kumbukumbu ya kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa kuchapa KMC FC kwa mikwaju ya penati mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha msaidizi wa Mbeya Kwanza FC Nizar Khalfan amesema heshima ni jambo kubwa sana kwao linapokuja suala la kupambana na washindani wao katika mchezo wa soka, hivyo Ruvu Shooting wanstahili hilo.

Amesema wanafahamu wenyeji wao wana uwezo mzuri na mkubwa kisoka, hivyo wamejiandaa kukabiliana nao kikamilifu ili kutimiza lengo la kuondoka na alama tatu katika Uwanja wa ugenini.

“Tumefika salama na tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa kesho Alhamis (Februari 03), tunaiheshimu Ruvu Shooting, na hii ni desturi yetu dhidi ya timu tunazokuna nazi kwenye mchezo wa soka,”

“Heshima dhidi ya wenyeji wetu haimaanishi unyonge dhidi yao, tupo hapa kwa ajili ya kushindana na tuna kikosi ambacho kinaweza kuikabili Ruvu Shooting na kuonesha maajabu ya kuondoka na alama tatu muhimu.” Amesema Nizar Khalfan

Mbeya Kwanza FC iliyoanza kwa makeke makubwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inakwenda kucheza dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 12 kwa kumiliki alama 12, huku wenyeji wao wakiwa nafasi ya 15 kwa kuwa na alama 11.

Ruvu Shooting yajizatiti kuibanjua Mbeya Kwanza
Kibu Denis kuikosa Tanzania Prisons