Wakati ukame ukiendelea kulikumba eneo la Pembe ya Afrika, kwa kipindi cha miaka 40 sasa, maelfu ya Wasomali wanaendelea kuvuka mpaka na kuingia nchini Kenya kutafuta maji na chakula kwa ajili ya wao na familia zao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), linasema zaidi ya Wasomali 80,000 tayari wamewasili Kenya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wakikimbia mchanganyiko tata wa migogoro na ukame.

Mzazi akiwa na wanawe katika moja ya maeneo ya Pembe ya Africa. Picha ya Cities Alliance

Wasomali hao, wengi wao wamelazimika kukimbia ghasia na kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na ukame, ulioletwa na misimu minne bila mvua na hali kama hii ulimwenguni, imekuwa ikiongezeka na kuyaathiri maeneo mengi.

Mmoja wa wahanga, Khadija Ahmed Osman (36), anasema aliamua kutoroka mji wa Buale na watoto wake wanane na kufika Dadaab mwezi Oktoba, 2022 na alilazimika kuachana na biashara yake ya hoteli kutokana na wakazi wengi pia kuukimbia mji huo kwa sababu ya ukame na pia kuepusha watoto wake kujiunga kwenye makundi ya silaha.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 10, 2022
Ya kale Dhahabu: Reli ya zaidi ya karne moja yaokoa usafirishaji