Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP , raia wa kusini mwa Madagascar wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju kwasababu ya kiangazi ambacho kimeharibu zao linalotegemewa na wenyeji .

“Tunauita udongo wenye kuhimili kiangazi kwasababu unaruhusu ukwaju kukua na kutusaidia kukabiliana na kiangazi,” AFP imemnukuu mkulima wa eneo Doday Fandilava Noelisona.


“Siku hizi hatutafuti tena chakula bali tunatafuta mbinu za kupata kitu chochote cha kushikilia tumbo.”

Matunda ya dungusi ambayo watu huyategemea yamekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua.

Aidha, shirika hilo limemnukuu mkulima mwingine, Avianay Idamy, ambaye anasema amegeukia uuzaji wa makaa kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia yake angalau waweze kula muhogo mara moja tu kwa siku.

Shirika la chakula dunia- WFP, linasema watu milioni 1.5 kusini mwa Madagascar wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Gattuso kusaini mkataba mpya SSC Napoli
EUROPA LEAGUE: Mourinho ashtukia jambo Spurs