Mradi wa Dunia wa Chakula (WFP), umeripoti kuwa njaa inayoikumba mataifa ya Yemen, Syria, Congo DRC na Sudan Kusini imepelekea watoto kulishwa udongo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema mzozo na njaa vinatakiwa kushughulikiwa pamoja kwa sababu vinakwenda sambamba

Katika Kikao kilichofanyika kwa njia ya video amesema njaa inapokutana na hali ya kutokuwa na usawa, matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi, shida za kimakundi huchochea mzozo

Mwaka 2020 watu millioni 80 waliteseka na tatizo la njaa lililotokana na mizozo na kutokuwa na utulivu.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Mwaka 2021 watu milioni 34 duniani wanashida kubwa ya chakula na wanahitaji msaada wa haraka.

Namungo FC kucheza viporo VPL
TCRA yatakiwa kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma