Vazi la brazia (sidilia) ni muhimu sana kwa mwanamke, nywele zako zinaweza kuwa nzuri na nguo zako zikawa nzuri lakini kuna kitu kidogo ambacho kina athari kubwa kwenye muonekano nacho ni brazia.
Kukosea kuvaa brazia kunaweza kuharibu muonekano wa mwanamke hata kama atakuwa amependeza usoni na mavazi ni muhimu kufahamu mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia vazi hili.
Vaa saizi yako.
hili ni jambo la muhimu sana katika uvaaji wa vazi hili, inashauriwa kuwa hakikisha kila kitu kinakaa mahali pake yaani haitakiwi kuvaa ndogo itakayofanya sehemu ya matiti kuchomoza nje, au kuvaa kubwa inayo pwaya na kuacha nafasi, kwa kuzingatia hilo utajiamini muda wote.
Usivae brazia nyeupe na nguo nyeusi
Inashauriwa kuwa katika kuchagua rangi ya brazia ya kuvaa hakikisha unaangalia rangi ya nguo yako unayotaka kuvaa kwa juu, kuvaa brazia nyeupe chini ya nguo nyeusi inayo angaza kutafanya watu waone brazia yako ya ndani kwani rangi nyeupe huonekana sana hali itakayo kufanya ukose uhuru pale watu watakapo kushangaa.
Usivae brazia za mikanda na nguo inayoonesha mabega
Kiuhalisia hakuna mtu anaye penda kuona nguo za ndani alizo vaa mwenzie, siyo ustaarabu kuonesha watu ndani umevaa nini, Brazia ni nguo ya ndani hivyo inashauriwa endapo utavaa nguo inayoenesha mabega hakikisha unavaa brazia ambazo hazina mikono.
Usivae brazia inayobana mgongo
imeelezwa kuwa uvaaji wa brazia inayobana sana una madhara kiafya, licha ya kusababisha maumivu ya mgongo, hupelekea mzunguko wa damu kusimama jambo ambalo ni hatari kiafya.
Usivae brazia chafu
Uvaaji wa brazia chafu hupelekea uginjwa wa fangasi chini na pembezoni ya maziwa, licha ya kuwa bado utafiti hauja onesha ni upi muda muafaka wa kufua brazia, inashauriwa kuwa endapo utaona brazia yako imechafuka usiivae kabisa.