Uzazi wa mpango ni maamuzi ya hiari ya mtu au mwenza juu ya ni wakati gani waanze kuzaa, watoto wangapi wazae, wapishane kwa umri gani na lini waache kuzaa, hivyo mtu anapotumia njia hizi humsaidia kuzuia kushika mimba.

Suala la uzazi wa mpango lilikuwa tangu enzi za zamani lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia mbinu zilizokuwa zikitumika miaka ya zamani tofauti na ambazo zinatumika miaka ya sasahivi ambapo kwa sasa wanawake hujikinga dhidi ya kupata ujauzito kwa kutumia mojawapo ya njia katika hizi; matumizi ya kondomu, njia ya vichecheo, njia ya sindano, Njia za Kizuizi, njia za asili, nijia za vipandikizi, kufunga uzazi kwa mwanaume, kufunga uzazi kwa mwanamke na kadhalika.

Hapa chini nimekuandalia njia asilia za kuzuia mimba bila kuhusisha vifaa wala kemikali ambazo watu wa zamani walikuwa wakizitumia kama njia yakujikinga kupata ujauzito kwa mujibu wa mtandao wa MedicineNet.

  1. Kinyesi cha mamba

Ndiyo dawa ya uzazi wa mpango ya kwanza kabisa duniani. Ilitumika Misri miaka 2000 K.K. Kinyesi kikavu cha mamba pamoja na asali kilikuwa kinawekwa ukeni, kinaachwa kilainike ili kutengeneza kizuizi kwa mbegu za kiume kuingia kwenye yai la mwanamke.

Na hii ni mojawapo ya njia ambayo ilikuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwani kinyesi cha mamba kina asidi ambayo husaidia kuua mbegu za kiume ambazo hurutubisha yai kwa mwanamke na kusababisha kushindwa kutungwa kwa mimba.

2. Kujifunga shingoni au mapajani kurodani za kicheche.

Mwanamke anashauriwa kuzifunga korodani hizo wakati akifanya mapenzi, njia hii pia iliaminiwa kusaidia kuzua mwanamke kushika mimba, lakiini pia unaweza kuzifunga kwenye mapaja huku ukiendelea kushiriki tendo.

3. Kupiga chafya na kufanya baadhi ya mazoezi.

Miaka ya zamani wafizikia kutoka Ugiriki walikuwa wanashauri mwanamke akishashiriki tendo la ndoa ili kuua mbegu za kiume anatakiwa kupiga chafya pamoja na kufanya zoezi na kusimama na kuchuchumaa kwa mara nyingi zaidi mara, lakini pia walikuwa wakishauriwa kuvuta pumzi kwa muda.

4. Kuchujia ndimu sehemu ya uke,

Hii njia ilikuwa inaaminikakuwa asidi iliyopo kwenye maji ya ndimu ilikuwa inasaidia kuua mbegu za kiume.

Japokuwa kwa asilimia kubwa njia hizi hazikuwa na mafanikio makubwa nyingi zilikuwa ziantegemea imani ya mtu, kama tulivyotambulisha hapo awali ukuaji wa teknolojia inakuwa na mambo yanabadilika hivyo kwa sasa zipo njia nyingi ambazo inashauriwa kutumika ili kujikinga na mimba zisizotarajiwa.

Na kwa mujibu wa majarida mbali mbali ya afya inashauriwa mwanamke kuanzia miaka 20 hadi 35 ndio umri sahihi wa kutumia njia za kisasa za mpango bila kujali kama umewahi kuzaa au hujawahi kuzaa.

 

 

 

 

Hali tete Rukwa Wanafunzi wa Sekondari wawapa Mimba wa Msingi
Panga - pangua ya Rais Magufuli yagonga vichwa, zengwe hatari kwa JPM