Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa njiti zinazotumika kusafishia masikio maarufu kama ‘Cotton Buds’, ndio chanzo cha ugonjwa wa masikio kwani zinaharibu ngoma ya masikio.

Waziri amesema hayo jana wakati akizindua mpango mkakati wa taifa kwa ajili ya masikio na usikivu kwa mwaka 2019 hadi 2023.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitahidi kutunza masikio, kuwa waangalifu na kushauri kutotumia dawa bila kuandikiwa na daktari.

Akisema hayo amezungumzia pia suala la vijana kutumia spika za masikioni ‘Earphone’ na kusema kuwa ndio chanzo cha tatizo la usikivu.

Ameongezea kuwa tatizo la sikio ni kubwa sana hapa nchini ambapo kati ya wagonjwa 100 wagonjwa 24 wanatatizo la usikivu.

Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo kwa kuweka miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa na wataalamu kwa njia ya kutoa huduma.

Ametolea mfano mwaka 2009 kulikuwa na wataalamu 11 wa magonjwa ya sikio ila hadi kufikia 2018 wameongezeka na kuwa wataalamu 46, lakini idadi hiyo bado haijitoshelezi kuhudumia watanzania milioni 50 waliopo nchini.

 

 

Kamishna Andengenye atoa somo kuhusu mitungi ya Gesi
Jeshi la Marekani limekiri ndege yake kutunguliwa na Iran