Njiwa aliyekuwa amebeba dawa za kulevya katika mkoba mdogo mgongoni amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kuwait.
Njiwa huyo amekamatwa jijini Abdali, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq baada ya kuzidiwa uzito, alikuwa amebeba jumla ya tembe 178 za dawa za kulevya aina ya Ketamine, nusukaputi katika mfuko huo uliokuwa umepachikwa mgongoni mwake.
Utumiaji wa Njiwa umeanza tangu enzi za Waroma kupeperusha ujumbe, lakini kwa sasa wamekuwa wakitumika na wafanyabiashara haramu kusafirisha dawa za kulevya hasa katika maeneo yenye ulinzi mkali.
Katika mwaka 2015, Askari magereza jijini Costa Rica walimkamata njiwa aliyekuwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Kokeni na Bangi, pia mwaka wa 2011, Jeshi la Polisi Colombia lilimkamata njiwa ambaye alishindwa kuruka juu ya ukuta mrefu wa jela kwa sababu ya uzito wa mzigo wa madawa ya kulevya.