Uongozi wa klabu ya Njombe Mji FC umewasilisha mapendekezo ya kutaka mchezo wao dhidi ya Simba upangiwe tarehe nyingine, baada ya tarehe mpya kutangazwa jana na afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura Mgoyo.

Njombe Mji FC wamethibitisha kuwasilisha mapendekezo hayo katika taarifa maalum iliyosambazwa katika vyombo vya habari na mkuu wa idara yao ya habari na mawasilino Hassan Macho.

Taarifa iliyotumwa na uongozi wa klabu hiyo inayosjhiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu inasomeka kama ifuatavyo.

Timu ya Njombe Mji FC inapenda kuujulisha umma wa Wananjombe na wapenda soka nchi nzima kuwa, tumepeleka mapendekezo yetu TFF na bodi ya ligi kuhusu taarifa ya ratiba tuliyoipokea jana saa 10 jioni ikionyesha mchezo kati yetu na simba utachezwa tarehe 3 Aprili 2018.

Katika mapendekezo yetu tumeishauri yafuatayo kwa TFF na TPBLB:-

  1. Baada ya michezo iliyokuwa kwenye ratiba inatoa nafasi katika kipindi cha siku 12 baada ya mchezo na Azam tarehe 15 Aprili, ingependeza mchezo ungechezwa hapo, badala ya kiporo cha Simba na Kagera Sugar kingefaa kuchezwa tarehe 3 mwezi wa 4 kwa timu zote hizo hazishiriki FA Cup.

 

  1. Kama ni lazima Simba icheze kiporo hiki basi mchezo huo tumependekeza ufanyike tarehe 30 au 31 mwezi wa tatu na mchezo wetu wa FA uliotakiwa kuchezwa tarehe 30 uchezwe tarehe 4.

Kwa kuwa barua yetu imefikishwa TFF na bodi ya ligi tunasubiri maamuzi ya busara kutoka TFF.

Ikumbukwe timu ilitakiwa kusafiri tarehe 27.3.2018 tukaamua kusitisha safari ili kwanza tupate muafaka.

Majibu yote yatapatikana baada ya barua kupata majibu.

Tuwaombe Wananjombe kuwa watulivu kipindi hiki ambacho tunashughulikia hali hii.

Imetolewa na

Hassan Macho

Msemaji wa Njombe Mji FC

27.3.2018

Kitenge chatakiwa kuwa vazi rasmi Afrika Mashariki badala ya suti
Mbowe na viongozi wake waswekwa mahabusu