Klabu ya Newcastle United imefanikiwa kumsajili kiungo kutoka nchini England, Jonjo Shelvey akitokea Swansea City.

Newcastle, wametumia kiasi cha pauni milioni 12 kumsajili kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23, kwa kuamini atasaidiana na wengine kumaliza tatizo la kusaka mafanikio kwa msimu huu.

Jonjo alifanyiwa vipimo vya afya na kufaulu katika hatua hiyo, na ndipo alisaini mkataba wa miaka mitano na nusu ambao utamuwezesha kuwepo St James Park hadi mwaka 2012.

Baada ya uhamisho huo kukamilika kocha mkuu wa kikosi cha Newcastle alimzungumzia mchezaji huyu na kusema “Ni mchezaji mwenye uzoefu katika nafasi ya kiungo wa kati nchini England.

Timu ya zamani ya Jonjo, Charlton,watapata kiasi cha mgao wa mchezaji huyo ambae alingara katika nafasi ya kiungo ya klabu ya Swansea msimu huu.

Andy Caroll Azusha Hofu Kubwa West Ham United
Picha: Majaliwa Amtembelea Sumaye Hospitalini