Mshambuliaji mpya wa Chelsea aliyesajiliwa kwa Pauni 52 milioni, Christopher Nkunku amefanyiwa upasuaji wa goti na atakuwa nje kwa miezi minne na atakosa mechi 13 ikiwemo dhidi ya Arsenal, Manchester City, Newcastle Aston Villa na Tottenham.

Hilo ni pigo kubwa kwa Chelsea kabla ya mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool. Mfaransa huyo alilazimika kutoka nje katika mechi ya kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund wiki iliyopita baada ya kuumia goti.

Chelsea ilikuwa na matumaini kwamba angekuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki kadhaa hata hivyo fowadi huyo atakuwa nje kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti. Kufuatia ripoti hiyo, Nkunku huenda akarudi dimbani Disemba.

KMC FC waivutia kasi Young Africans
Simba SC yawabana Onyango, Kyombo