Mcheza Tennis raia wa Hispania Rafael Nadal amemvua ubingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open) Novak Djokovic kwa kumfunga kwenye mchezo wa Robo Fainali usiku wa kuamkia leo.

Nadal ambaye ni bingwa mara 13 wa michuano hii ameshinda mchezo huo kwa seti 3-1 kwa ushindi wa seti 6-2 4-6 6-2 7-6 mchezo uliochezwa kwa masaa 4. huu pia ni ushindi wa 29 kwa Nadal dhidi ya Djokovic kwenye michezo 59 waliokutana huku Djokovic akiwa ameshinda mara 30.

Katika hatua ya Nusu Fainali Rafael Nadal atacheza dhidi ya Alexander Zverev keshokutwa Ijumaa, Zverev ametinga hatua ya Nusu Fainali kwa kumnyuka Carlos Alcaraz kwenye mchezo wa Robo Fainali kwa seti 6-4 6-4 4-6 7-6 (9-7).

Serikali kuajiri askari 600 kukabiliana na wanyama
Simba SC mjihadhari na MAFISI WA MPIRA