Aliyekua nahodha na kiungo wa timu ya taifa ya Rwanda ‘AMAVUBI’ Haruna Niyonzima ametuma salamu kwa mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kwa kuwataka wajiandae kisaikolojia kuhusu taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

Niyonzima ambaye aliwahi kuitumika Simba SC kwa msimu miwili kabla ya kurejea Young Africans, amesema kikosi chao kipo tayari kwa mapambano ya kuwania taji la Ligi Kuu, na anaamini watafanikiwa.

Kiungo huyo ambaye juma lililopita alitangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Rwanda ‘AMAVUBI’ amesema wadau wengi wa soka nchini wamekua wakiamini huenda Young Afrcans wakashindwa kufikia lengo la kutwaa taji la Tanzania Bara msimu huu, lakini kwake kama mchezaji mwenye uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu, anafikiria tofauti.

“Kwa jinsi tulivyojipanga mwaka huu ni wakati wa kumaliza ufalme wa watani zetu Simba SC ambao wametwaa taji la Ligu Kuu mara tatu mfululizo,”

“Tuna uzoefu mkubwa na Ligi Kuu Tanzania Bara, mzunguko wa pili umekuwa na hesabu sana na sisi tumejipanga kuhakikisha tunamaliza michezo tukiwa kileleni na kushinda taji,” amesema Niyonzima

Young Africans itaendelea na MShike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili kwa kucheza dhidi ya KMC FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 50 huku ikicheza michezo 23, Simba SC ambao ndio mabingwa watetezi wanashika nafasi ta pili kwenye msimamo huo wamefikisha alama 46 wakicheza michezo 20, huku Azam FC wakishika nafasi ta tatu kwa kufikisha alama 44 baada ya kucheza michezo 24.

Manula: Simba SC ina malengo makubwa CAF
Rais Samia awataka watendaji kuwajibika, "Ukinizingua tutazinguana"