Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza jana (Desemba 03) jioni alianza mazoezi rasmi na kikosi cha Young Africans, baada ya kuwasili nchini juzi Jumanne akitokea nchini kwao.

Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kucheza soka nchini Ufaransa na Uholanzi, amesema amefurahuia kujiunga na wachezaji wa Young Africans, na ana hamu kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kwenye harakati za kusaka ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

“Kawaida huwa sipendi kuwa muongeaji sana kazi yangu ndio itazungumza uwanjani, nimeanza mazoezi na wachezaji wenzangu, hatua hii imenifurahisha sana na nipende kuwaahidi mashabiki kuwa subra, wataniona nikicheza kwa bidii.”

“Kila mmoja hapa mazoezini yupo vizuri sana, jambo hili limenihamasisha kupambana nikiwa hapa, maana inaonekana kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ni changamoto.” Alisema mshambuliaji huyo baada ya kukamilisha mazoezi ya jana jioni.

Ntibazonkiza ataanza kuitumikia Young African katika michezo ya Ligi kuu na Kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usalaji Desemba 15.

Ntibazonkiza alisajiliwa na Young Africans siku chache baada ya kuja Tanzania kucheza na Taifa Stars akiwa na kikosi cha Intamba Murugamba (Burundi) katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, ambao alifunga bao pekee.

Ndugai: Tutazame upya masharti ya mikopo kwa walemavu
Mfumo bora wa hakimiliki kuwainua wasanii