Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Young Africans Antonio Nugaz amesema kuwa baada ya klabu hiyo kupoteza mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC Jumapili (Julai 25) mjini Kigoma, hakulala kwa siku tatu.
Nugaz amefichua siri hiyo alipohojiwa kwenye kipindi cha The Empire cha Radio E FM jana Alhamisi (Julai 29) jioni, huku akisema mbali na kushindwa kupata usingizi, pia alilazwa hospitali baada ya mchezo huo.
“Nilipata wakati mgumu sana baada ya ule mchezo, sikuamini kilichotokea na nikwambieni ukweli tu, sikulala siku tatu kwa sababu niliumia sana,”
“Ligine ambalo wengi hamlijui ni kwamba nililazwa hospitali, Iliniotea kweli ile, imeniuma, sijalala siku tatu, Young Africans inauma usichukulie poa, Young Africans kwangu mimi sio kazi ni maisha nikiwa ndani ya Young Africans na nikiwa nje ya Young Africans.” alisema Antonio Nugaz
Young Africans walipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba SC, bao likifungwa kwa kichwa na kutoka nchini Uganda Thadeo Lwanga akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa kutoka Msumbiji, Jose Luis Miquissone.