Wikendi iliyopita zilisambaa sauti za mazungumzo ya simu zilizoaminika kuwa ni mazungumzo kati ya Nuh Mziwanda na Wema Sepetu ambapo Nuh alisikika akimbembeleza Wema awe mpenzi wake.

Leo, Nuh ambaye ni mpenzi wa Shilole amezungumza na Bongo5 na kukanusha sauti hiyo akidai imetengezwa kwa lengo la kuwaharibia.

“Ile sio sauti yangu watu tu wameamua kufanya ili kunichafulia mimi labda na mpenzi wangu. Kwa sababu ukisikiliza mwishoni kuna mtu amejitaja jina lake. Ni kitu ambacho kimepelekwa studio wakaiweka sawa ili wapate kitu kibaya kije kwangu na Shishi. Hiki kitu sikukitegemea kwa sababu watu waliofanya kitu kama hicho ni watu ambao kwenye vitu vingi, kwenye mambo ya kampeni yaani mimi sijategemea,”alisema Nuh Mziwanda.

“Mimi hili suala nalichukulia kawaida na naona ni ushamba na upu*vu na hawana akili hata kidogo. Kama ni kweli, angemfuata Shishi akamwambia kwamba mpenzi wako kafanya kitu fulani fulani kwangu’ sio kutangaza. Na kama kweli, kwanini asingesema wengine wanaomtongoza na akawaweka mtandaoni? Ni Wema pamoja na watu wake wote ndio wamefanya hivi! Siku ya kwanza Shishi alilipokea vibaya lakini baada ya kumuelewesha kanielewa,” aliongeza.

Kwa upande wa Shilole ambaye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti yaliandika kuwa alizimia baada ya kusikia sauti ya Nuh na Wema Sepetu, alitoa ya moyoni akidai kuwa kweli alishtushwa na tukio hilo lakini baada ya kusikiliza utetezi wa Nuh amemuelewa na kumsamehe.

“Mimi sina ugomvi na mtu katika maisha yangu. Kama wametengeneza ili wafanye hayo yote mimi sijali, watajua wenyewe, of course limeathiri mapenzi yetu. Sasa hivi tupo fresh, kwasababu mwenyewe ameshaniomba ‘mpenzi wangu msamahani kwa kilichotokea lakini sio kweli’  Nimeshamsamehe, mimi nimemuelewa alichosema Nuh,” alisema Shilole.

Benitez Azifanyia Kauzibe Man Utd, Arsenal
Dk. Slaa Kuiokoa Chadema Dhidi Ya Mtego Wa CCM?