Kwa nuhu siyo ishu kubwa kuchora tattoo za wapenzi wake inaweza ikawani njia mojawapo ya kuonesha mapenzi, akiwa bado hajafuta tattoo ya aliyekuwa mpenzi wake ”Shishi beibe” tayari nuhu mkononi ameweka nyingine ya Mpenzi wake wa sasa.

Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amechora tattoo mpya katika mkono wake wa kushoto ya jina la mpenzi wake wa sasa aitwae ‘Nawal’.

 

Nuh akiwa na mpenzi wake mpya aitwae Nawal
Nuh akiwa na mpenzi wake mpya aitwae Nawal

Mwimbaji huyo ambaye bado ana tattoo nyingine mkononi ya mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds TV kuwa, haoni kama ni tatizo kuchora tattoo ya mpenzi wake huyo.

“Yeah nimechora (huku akiionyesha) nimempenda na yeye ananipenda,” alisema Nuh. “Huyu ana mapenzi ya dhati kwangu, Shilole alikuwa hataki niwe na washkaji, yaani nikae ndani tu hata mwaka mzima, lakini kwa mpenzi wangu huyu yupo poa sana, anawapenda marafiki zangu, anawapikia geto tunakula, kwa hiyo kwangu mimi tattoo ni kama ndoa,”
kk
Nuh na Mpenzi wake

Kwa upande wa mpenzi wake huyo aitwae, ‘Nawal’ alisema anafurahi kuwa na Nuh.

“Ananipenda na mimi nampenda, sioni tatizo kuchora tattoo kwa ajili yangu,” alisema Nawal.

.com sasa

Chris Brown amuokoa Shabiki aliyetaka kujitoa roho
Mh.Zambi atembelea miradi mbalimbali wilayani Ruangwa