Dirisha la usajili la Ligi ya Kulipwa ya Saudi Arabia lilifungwa rasmi juzi Alhamis (Septemba 07) na kukamilisha rekodi ya matumizi ya fedha, lakini Al-Ittilhad imeshindwa kutimiza lengo lake la kumuondoa Mohamed Salah katika klabu ya Liverpool.

Kikosi hicho cha Kocha Nuno Espirito Santo awali kiliwasilisha ombi la kiasi cha Pauni 150 ambalo lilikataliwa na Liverpool.

Ilidaiwa kuwa klabu hiyo Saudi Arabia ilikuwa tayari kuweka mezani kiasi cha Pauni milioni 200 ambalo pia lilikataliwa huku lle la Pauni milioni 215 ambalo lingekuwa rekodi ya dunia, halikuthibitishwa.

Makocha wengi wa Ligi Kuu ya England walikosoa tarehe ya mwisho ya usajili wa Ligi ya Saudi Arabia juma moja baada ya kukamilika kwa ule wa ligi kubwa za Ulaya.

Awali, kulikuwa na wasiwasi kuwa Al-Ittihad wangeweza kuja na ofa nono kwa ajili ya kumnasa Salah kwani wangeshindwa kumnunua mbadala wake katika kipindi cha miezi minne.

Salah alifunga mabao 188 katika mechi 309 hapo Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Roma mnwaka 2017.

Watoto mapacha wa mwaka mmoja wavikwa vilipuzi
Imarisheni mifumo kuwalinda Wafanyakazi - Majaliwa