Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amedai kuwa Waziri wa sasa wa wizara hiyo Dkt. Hamisi Kigwangalla anatumika vibaya katika kumchafua na kueneza uzushi juu ya utumishi wake.

Ameyasema hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa anasikitika kuona waziri huyo ametumia muda wake ndani ya bunge kumchafua, pamoja na kusema uongo dhidi yake ikiwa anatambua kuwa ni njama za makusudi zilizopangwa kumchafua baada ya kuhama ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Amesema kuwa kinachofanywa juu yake ni hatua ambayo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama hicho.

“Kigwangallah anatumika vibaya, kwa kueneza uongo na uzushi aliouanza dhidi yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya utumishi wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye rekodi thabiti,”amesema Nyalandu

Hata hivyo, kati ya habari ambazo Nyalandu amedai kuwa ni za uzushi ni pamoja na ile aliyoisema Dkt Kigwangalla bungeni kwamba kiongozi huyo alikuwa akitumia helikopta kugombea urais 2015 kitu ambacho Nyalandu amekipinga.

Jeshi ‘labisha hodi’ mgogoro wa madaraka Zimbabwe
Video: Vita mpya yaibuka kati ya Nyalandu na Kigwangalla, Zito njia panda...