Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na wengine watatu mapema leo wameripoti kituo cha polisi mkoani Singida na kutakiwa kuruudi tena polisi ifikapo Mei 31, 2019.
Ambapo nusu saa baada ya kufika kituoni hapo walichukuliwa na maofisa wa takukuru na kuhojiwa kwa takribani saa moja na kisha kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kwa kila mmoja.
Nyalandu amesema polisi imewataka kuripoti kituoni hapo siku ya ijumaa huku watu wa Takukuru wakiwataka kuripoti Juni 19 mwaka huu.
Aidha Nyalandu amewaomba makamanda wa Chadema na wanachama wote wa Chadema kuwa na utulivu sana katika kipindi hiki na amewaomba wasilipize ubaya kwa ubaya bali ubaya kwa uzuri.
Aidha Nyalandu alikamatwa na Takukuru siku ya jumatatu ya Mei 27, 2019 katika kata ya Itaja jimbo la Singida Kaskazini akituhumiwa kwa makosa mawili ya rushwa na kuendesha kmkutano bila kibali.