waziri wa zamani wa Maliasili na utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu umezuiliwa kuvuka mpaka wa Namanga kuingia Nchini kenya.
kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, amesema Nyarandu ambae alikuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA, tiketi yake ya kusafiria haikuwa imeambatanishwa na taarifa muhimu.
“Ni kweli kuwa Mamlaka ya Uhamiaji inamshikilia kwa kukosa taarifa nyingi muhimu ambazo zinampa ruhusa ya kuondoka” amesema Mwaisumbe.
Amesema kuwa waziri huyo wa zamani alihitajika kukamilisha taarifa zake ndipo aweze kuachiwa huru eneo hilo la Namanga.
“Tumemtaka kuleta nyaraka muhimu lakini akishindwa tutamfikisha mahakamani” aliongeza
Zuio la Nyalandu kuvuka mpaka linakuja siku mbili baada ya mbunge wa zamani jimbo la Arusha Godbless Lema, kuripotiwa kuondoka nchini na kushikiliwa nchini kenya baada ya kuingia bila ya Nyaraka muhimu.
Akizungumza na kituo cha habari cha The Nation ya kenya mwanansheria wa Lema, George Luchiri amesema mwanasiasa huyo anatafuta makazi nchini humo.