Hali ya sintofahamu imeibuka miongoni mwa viongozi, mashabiki pamoja na wachezaji wa klabu ya Villarreal baada ya mshambuliaji wa klabu hiyo Roberto Soldado kuumia goti akiwa katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini Hispania dhidi ya Deportivo la Coruna uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Mshambuliaji huyo alilazimika kutolewa uwanjani akiwa amebebwa kwenye machela na nafasi yake kuchukuliwa na Teresa Herrera katika dakika ya 13, baada ya kushindwa kuumiliki vyema mpira na kupelekea kuanguka vibaya.

Meneja wa Villarreal, Marcelino amesema kuna wasiwasi mkubwa kwa mshambuliaji huyo kurejea mapema uwanjani, kutokana na jeraha alilolipata.

Amesema alikua ameshamuandaa kwa ajili ya mchezo wa hatua ya mtoano wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya AS Monaco utakaochezwa juma lijalo, na sasa hana budi kusubiri taarifa za kitabibu.


Hata hivyo majibu ya vipimo alivyofanyiwa Soldado, ndio yatatoa mustakabali mzuri wa matarajio ya kutumiwa katika kikosi cha Villarreal katika michezo ya mwanzo ya msimu ujao ama kusubiri kwa muda mrefu akiwa nje ya uwanja.

Katika mchezo huo wa kirafiki Villarreal walikubali kupoteza kwa mabao mawili kwa sifuri, yaliyofungwa na Florin Andone na Carles Gil katika dakika ya 7 na 90.

Claudio Ranieri Ajiongeza Hadi 2020
Shkodran Mustafi Aondolewa Kikosini