Nyani anayedhaniwa kuwa ni kichaa amevamia kijiji cha Msungua mkoani Singida na kuingia katika nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, kisha kuanza kula chakula ambacho ni kiporo kilichokuwa kimehifadhiwa sanjari na kumjeruhi vibaya Jumanne Makiya aliyetaka kumshambulia kwa kutumia shoka.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya asubuhi ambapo nyani mkubwa alifanikiwa kuingia kwenye nyumba ya Jumanne, ndipo mwenye nyumba alipomkuta nyani huyo anakula chakula chake, akatoka nje na kuanza kupiga mayowe kuomba msaada kwa majirani.
Majirani walipofika walimkuta Nyani huyo ametoka nje na kukaa kwenye kisusi cha nyumba, walipoanza kumfukuza akakimbilia kwenye kichaka cha miba kilichokuwa karibu na kujificha, ndipo walipozingira kichaka hicho wakiwa na silaha pamoja na Mbwa, kwaajili ya kumkabili Nyani huyo.
Walipo zidi kusogelea kichaka hicho, Nyani akaanza kuwa mkali kwa kuunguruma, katika purukushani hizo , Mgosha alifika na shoka kwa lengo la kumkata lakini baadaye alianguka na kumpa nafasi nyani huyo amshambulie , kwa kmchana na kucha zake.
-
Urusi yamkamata mpelelezi wa Marekani
-
HapoKale: Kabila lenye utani na makabila mengi isipokuwa Wamasai
Wakati mapambano yanaendelea majirani kwakujihami walikimbia, Mgosha alifanikiwa kuokolewa na Mbwa ambao walimshambulia Nyani huyo aliyekimbia na kutokomea msituni.
Mganga mkuu wa zahanati ambayo majeruhi alikimbizwa, ameeleza kuwa alifikishwa saa 6:00 mchana akiwa na majeraha makubwa mikono yote na mengine kifuani,shingoni, na tumboni, ambapo alishonwa nyuzi nane na kupelekwa kituo cha Afya Sepuka na baadaye Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa tiba zaidi.
Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Msungua, Omari Bayyu , amethibitisha kuwa na taarifa za muda mrefu juu ya Nyani huyo kuzunguka kwenye makazi ya watu na katoa tahadhari kupitia kwa Wenyeviti wa vitongoji wa maeneo hayo iwapo atatokea taarifa zitolewe haraka adhibitiwe ili asilete madhara zaidi kwa watu.