Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amekanusha mashtaka ya kuhifadhi kinyume cha sheria mamia ya nyaraka za siri za serikali, baada ya kuondoka Ikulu na kuzuia juhudi za serikali kuzipata.

Trump aliweka historia wiki iliyopita wakati jopo la mahakama lilipomshtaki kwa makosa 37 ya uhalifu, yakiwemo makosa 31 ya kuhifadhi kwa makusudi taarifa za siri za ulinzi wa taifa, huko Mar-a-Lago, katika makazi yake jimboni Florida.

Kushtakiwa kwa rais huyo wa zamani kulifanyika chini ya ulinzi mkali, huku mamia ya wafuasi wa Trump wakikusanyika nje ya Mahakama na mbele ya hakimu wa serikali kuu mjini Miami, Florida Trump alikanusha madai hayo,.

Kenya: Idadi ya waliofariki mfungo tata yafikia watu 303
Wafanyabiashara Austria waitwa kuwekeza nchini