Jeshi la Polisi limefanya upekuzi Makao Makuu ya Chama cha ACT- Wazalendo na kuchukua nyaraka, vifaa vya kielektoniki vilivyotumika kuandaa taarifa ya kusinyaa kwa uchumi wa nchi.

Upekuzi huo umefanyika baada ya siku chache, Zitto kutakiwa kwenda kuripoti Kitengo cha Uhalifu wa Makosa ya Kifedha Kamata jijini Dar es salaam na kutakiwa kurejea tena Novemba 21.

Aidha, katika Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema kuwa polisi walifika ofisini hapo kwaaajili ya kufanya upekuzi na kuondoka na  flash, Laptop (kompyuta mpakato) na nyaraka ambazo ni taarifa kwa umma iliyotolewa kupitia wanahabari.

“Wamesema watakwenda kufanyia kazi vifaa hivyo na watavirejesha haraka ila hawajasema hasa ni lini watavirejesha, hivyo tunasubiri chochote kitakachotokea,” amesema Ado Shaibu.

Hata hivyo, Jeshi hilo la polisi lilishikilia simu ya mkononi ya Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa upelelezi huku yeye akisema mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yamezingatia uhuru ulipo katika Katiba

Ng'ombe 692 wakutwa wamekufa
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 8, 2017