Serikali imesitisha nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma, utoaji wa ajira mpya pamoja na utoaji wa vibali vya likizo bila malipo.

Taarifa zilizothibitishwa na Katibu Mkuu wa Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro zimeeleza kuwa lengo la kusimamishwa kwa utaratibu huo ni kupitia upya muundo wa ajira Serikali Kuu na katika Taasisi zake zote ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la watumishi hewa.

“Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitiaa mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki,” Dk. Ndumbaro amekaririwa na gazeti la Mtanzania.

Waraka wa Serikali umeeleza kuwa utaratibu wa watumishi wa umma kuhama kazi katika taasisi fulani ya umma na kuhamia taasisi nyingine ya umma kufuata ongezeko la mshahara umesitishwa pia.

Watumishi wa umma waalikuwa wakisubiri ongezeko la kila mwaka la mishahara yao pamoja na stahiki zilizofanyiwa marekebisho kwa baadhi ya taasisi kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha 2016/17, ambapo walikuwa wakisubiri kupitishwa kwa bajeti husika.

 

Ukawa watoka bungeni wakijifunga midomo, Mbatia afunguka
Quincy Promes Kuwa Mbadala Wa Vardy Emirates Stadium