Beki na nahodha wa klabu ya Mbeya City, Juma Said Nyosso amesema hakumbuki kama alimfanyia kitendo cha utovu wa nidhamu mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Azam FC John Bocco.

Nyosso, alisema hayo jana alipofanyiwa mahojiano na muandishi wa habari za kituo cha Azam TV, ambapo alibainisha huenda kitendo hicho kikawa kimetengenezwa kwa makusudi ya kumkandamiza, kutokana na makosa aliyowahi kuyafanya siku za nyuma.

Kwa kuhofia jambo hilo, beki huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Ashanti Utd, Simba pamoja na Costal Union kabla ya kusajiliwa na Mbeya City, ameutaka uongozi wa chama cha wachezaji wa soka SPUTANZA kumsimamia na kumtetea katika sakata hilo ambalo limemuingiza kwenye kifungo cha miaka miwili sambamba na kutozwa faini ya shilingi million mbili.

“Sikumbuki kufanya hivyo, huenda watu wananihukumu kwa yale niliyofanya nyumba,” alisema.

Naye kocha mkuu wa Mbeya City, Juma mwambusi alisema amejaribu kuufuatili mchezo wa Azam FC dhidi ya kikosi chake kwa njia ya televisheni na kubaini hakukua na kosa kama hilo, hivyo ameziomba mamlaka za soka kutenda haki dhidi ya Nyosso.

“Siung mkono vitendo vya utovu wa nidhamu kwa mchezaji wangu yoyote anapokua ndani na nje ya uwanja, hivyo nitakua mpuuzi kama nitamtetea Nyosso kwa kosa ambalo anadaiwa kulifanya, wakati mimi ni muumini wa nidhamu siku zote” Alisema Juma Mwambusi.

Katika hatua nyingine Mwambusia meahidi kumtumia Juma Nyosso katika mchezo wa hii leo dhidi ya Toto African utakaochezwa jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba, kwa madai hajapokea taarifa rasmi kutoka bodi ya ligi.

 

Baada Ya Ushindi, Mashabiki Wa Simba Wapongezwa
Mbatia Aeleza Njama Za Kutaka Kuuawa Na Kudhoofisha Ukawa