Kiungo kutoka nchini Ufaransa, Vassiriki Abou Diaby huenda akaonekana tena katika ligi ya nchini Uingereza msimu ujao baada ya kutupiwa virago na klabu ya Arsenal iliyokuwa ikimmiliki kwa zaidi ya miaka saba iliyopita.

Kiungo huyo ambaye alishindwa kucheza mara kwa mara kutokana na majeraha ya mguu aliyoyapata mwaka 2007, ameripotiwa kuwa katika mazungumzo na meneja wa klabu ya West Brom, Tony Pulis.

Mazungumzo baina ya wawili hao yapo katika hali nzuri, Abou Diaby amerejea kwenye hali yake ya kawaida kiafya na imethibitika kuwa yupo tayari kupambana kama ilivyokua zamani.

Pulis anaamini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, bado ana nafasi ya kuonyesha uwezo wake kisoka na kuisaidia West Brom, hivyo ana matumaini ya kufikia muafaka mzuri katika mustakabali wa kukisuka kikosi chake.

Josep Bartomeu: Vyombo Vya Habari Acheni Uzushi
Urusi Yatahadharishwa Kombe La Dunia 2018