Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga Kigoma imeungua moto jioni ya leo ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa chama cha ACT, Abdalla Khamis na kusema ni kweli tukio hilo limetokea lakini siyo katika nyumba ambayo aliyokuwa anaishi Zitto.

“Ni kweli nyumba ya Zitto imeungua moto jioni ya leo lakini siyo nyumba ambayo anaishi yeye binafsi, bali ni nyumba ambayo imejengwa katika kiwanja kimoja na nyumba anayoishi kwa sasa,”amesema Khamis

Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu
Man City yapaa kileleni EPL, yaibamiza Watford