Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa, amewata viongozi wa dini kutotumika kumfanyia kampeni mgombea yeyote wa chama cha siasa kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki waumini wake.

Ametoa agizo hilo leo Septemba 26, 2020, jijini Dar es salaam, wakati wakizungumza na wandishi wa habari ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya amani Sheikh Alhadi Mussa Salum, amesema kwa kufanya hivyo inawezekana ikawa chanzo cha kuvuruga amani ya nchi.

“Muacheni mtu akamchague kiongozi anayemtaka na sio wewe kiongozi wa dini fulani unatumia nyumba za ibada kama ni jukwaa la kisiasa,” amesema mwenyekiti wa kamati hiyo Shekh Salum.

Aidha amewataka viongozi wa dini kutoshirikiana katika kupinga kutumia nyumba za ibada kunadi sera zao.

“Nimesikitishwa sana”- Kikeke
Ruksa kuanzisha Bucha ya nyamapori