Wanafainali ya Europa League msimu wa 2016/17 klabu ya Ajax Amsterdam, wamemsajili kwa mara nyingine mshambuliaji wake wa zamani Klaas-Jan Huntelaar, ambaye amemaliza mkataba na FC Schalke 04 ya Ujerumani.

Huntelaar mwenye umri wa miaka 33 amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo aliyoihama miaka minane iliyopita.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Uholanzi, alijiunga na Ajax kwa mara ya kwanza Januari 2006 kabla ya kutimkia kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrdi mwaka 2009. Akiwa na Ajax, Huntelaar alifanikiwa kufunga mabao 105 katika michezo 137.

Ajax imemsajili Huntelaar ili kuiongezea makali safu ya ushambuliaji ambayo kwa msimu uliopita ilishindwa kufikia lengo la kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Eredivisie tangu mwaka 2014.

Juma Mahadhi Ashtuka, Aomba Kuondoka Young Africans
Simba SC Yapandisha Thamani Ya Usajili Wa Wachezaji