Waziri wa Kilimo wa Sudan Kusini, Onyoti Adigo amesema nchi hiyo imekumbwa na uvamizi wa Nzige.
Wadudu hao wameonekana katika jimbo la Equatoria karibu na mipaka ya Ethiopia, Kenya na Uganda, ambazo pia zimeathiriwa na wadudu hao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Waziri Adigo amesema Mamlaka zitajaribu kudhibiti nzige hao ambao idadi yao inakadiriwa kufikia 2,000.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini humo, Meshack Malo, amesema endapo nzige hao watashindwa kuthibitiwa, Sudani Kusini inaweza kuingia matatizoni kwani nusu ya wananchi tayari wanakabiliwa na baa la njaa baada ya miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.