Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa atahakikisha kuwa wale waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki wanakamatwa na kushitashtakiwa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na rais Recep Tayyip Erdogan kandokando ya mkutano wa G-20 mjini Hangzhou nchini China.

Uturuki inadai kuwa kiongozi wa dini mwenye makao yake huko Marekani Fethullah Gulen ndiye aliyepanga njama ya mapinduzi hayo na inataka arudishwe nchini Uturuki

Lakini rais Obama hakuzungumzia kuhusu swala la kumrudisha Uturuki kiongozi huyo.

Bwana Gulen amekana kuhusika na jaribio hilo.Rais Obama na Erdogan pia walizungumzia kuhusu hali ilivyo nchini Syria

Uhuru Kenyata Akanusha Kuwepo Mvutano Wa Kiuchumi Kati Ya Tanzania Na Kenya
Aguero Kuikosi Derby Na Watani Zao Man u