Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ameunga mkono utawala wa Rais wa Marekani joe Biden wa kupitisha bajeti ya dola bilioni 555 katika kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Rais mstaafu obama ameuunga mkono suala hilo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kujadili athari za mabadiliko ya tabia nchi, huku akizikosoa China na Urusi kwa kile alichokiita kutojitolea kwao katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafu inayochafua mazingira.

Obama ambaye ni mmoja wa viongozi waliohusika kwa kiasi kikubwa katika kupitishwa mkataba wa kihistoaria wa mabadiliko ya tabia nchi uliotiwa saini mjini Paris mwaka 2015, licha ya kuwa na matumaini na majadiliano yanayoendelea kwenye mkutano huo wa Cop 26, amekiri kuwa na mashaka juu ya maisha ya baadaye.

Kauli yake imetokea wakati viongozi kwenye mkutano huo wakikiri kuwepo kwa tofauti za wazi miongoni mwao baada ya wiki nzima ya mazungumzo.

Aidha Rais Mstaafu Obama ametoa wito kwa wanaharakati vijana wa mazingira kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia na kuzitaka nchi tajiri kumaliza mkwamo juu ya ufadhili wa mazingira. 

Jua la utosi chanzo cha joto kuongezeka
Tanzania, Mauritius wateta Diplomasia ta Uchumi