Bilionea anaewania nafasi ya kuwa rais wa Marekani, Donald Trump, jana aliwashukia Rais Barack Obama na Bi. Hillary Clinton kuwa  ndio waliolitengeneza kundi la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq na Syria (ISIS).

Donald Trump

Donald Trump

Trump alieleza kuwa sera za mambo ya nje za rais Barack Obama na Bi. Clinton ndizo zilizosaidia kulisuka kundi la ISIS na kuhatarisha usalama wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi.

“Walitengeneza ISIS, Hillary Clinton alitengeneza ISIS na Obama,” Trump anakaririwa.

Akitoa ushahidi wa alichokieleza, Trump alidai kuwa mvutano uliopo hivi sasa kati ya Saudi Arabia na Iran unaonesha dhahiri kuwa Jamhuri ya Kiislam ilitaka kuchukua washirika wote wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

“Huko Tehran, wanachoma ubalozi wa Saudi Arabia, mnaona..? alihoji. “Hii ni ishara kuwa Iran inataka kuichukua Saudi Arabia kama mshirika wake. Wanataka kufanya hivyo siku zote, wanahitaji mafuta,” aliongeza.

 

Meya auawa Siku Moja baada ya Kula Kiapo
Ligi Ya England Kuendelea Wikiendi Hii