Baada ya kuchafua hewa mapema leo kwa maandishi yaliyochukuliwa kama dharau kwa mwimbaji ‘Wahu’ ambaye ni mke wa Nameless, Rapa Octopizzo amejitokeza na kutoa ufafanuzi wa kauli yake huku akiwaomba radhi wana familia hao.

Nameless, wahu na Octopizzo

Octopizzo ameeleza kupitia Facebook kuwa amefanya mahojiano na Kiss Radio ya nchini humo na kuzungumza na Nameless kwa njia ya simu na kuweka sawa hali ya sintofahamu iliyokuwa imejitokeza.

Rapa huyo ameeleza kuwa yeye amekuwa shabiki wa Wahu tangu akiwa na umri wa miaka 8 na kwamba ataendelea kuwa shabiki wake na kumpigia kura kwenye Tuzo zozote za Kenya.

“Thanks to Kiss Radio & Nameless for Calling me and clearing up the misunderstanding.
Now let’s change the face of the awards in this Country together for the Love of our Art.
I respect Nameless & Respect Wahu been a fan since class 8 & still a fan & will vote for Wahu anyday & not only her but all the female artists out there,I’ll always fight for you Queens Beli’Dat!
And thanks for my fans for staying being Loyal ?‪#‎teamocto‬ #808 ‪#‎love‬‪#‎Music‬ ‪#‎Growth‬ ‪#‎change‬ ‪#‎changethesystem‬ ‪#‎dontbeafraid‬,” Octopizzo ameandika Facebook.

Hata hivyo, rapa huyo aliendelea kusisitiza kuwa hataikubali tuzo ya “comeback” kwa sababu anaamini hajawahi kukaa kimya katika muziki na baadae kurudi kama inavyotafsiriwa na tuzo hiyo.

Kiwanda cha muziki cha Kenya kilikuwa na mada moja nzito kuhusu ‘bifu’ la ghafla lililoibuka kati ya Nameless na rapper Otopizzo, baada ya rapa huyo kutoka Kibera kuonesha kutoikubali tuzo ya Bingwa kwa madai kuwa haimfai na kupendekeza angepewa ‘Wahu’.

Jumamosi iliyopita, Otopizzo aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Facebook:

“Thanks for ‪#‎BingwaAwards‬ for the Award last Night,unfortunately I won’t take the award of “ComeBack Artist Of The Year” I never went anywhere,I’ve been here since my 1st hit single OnTop,I put in more work than any artist of my Genre ,unless you are awarding me for coming back from my Europe tour then it doesn’t make sense ,I never understand awards in this Country,I’d rather you acknowledge & Respect my work than award me & nominating me for a “comeback” Award which was such a joke,so if you don’t mind plizz give my award to Wahu who was in the same category. Next time you nominate me please make sure you do a background check of my catalogue;The Quality of Hip hop music when it comes to Audio & video that I’ve brought to this industry since I stepped in. You can’t compare to any not even close,All in all I wish you the best and congrats to the “Winners” last night,& we still have along way to go as far as awards are concerned.
OCTO
‪#‎IdontWantTheAward‬ ‪#‎iwantrespect‬ ‪#‎music‬ ‪#‎awards‬ ‪#‎hiphop‬ ‪#‎ikeepitreal‬‪#‎trill‬ ‪#‎doer‬

Naye Nameless alishindwa kuvumilia kauli hizo na kuamua kumjibu msanii huyo akimchana kuwa amemkosea sana Wahu kwa kumshusha na alimtaka amheshimu.

“@wahukagwi ebu check this guy out. He says he is too big to receive this award!He even recommended that it be given to you, joyjoyjoyjoy!! Bro, let me give you advice; Appreciate and receive these awards that you win now, because there can come a time in your career that you don’t even get noticed or nominated, ameandika Nameless kwenye Instagram. But I am sure you too big to receive advice , ama? Lakini seriously, you belittle the award then you recommend it to be given to Wahu?? Tuheshimiane;  humble yourself before life humbles you.” Nameless alimjibu Octopizzo.

 

 

 

China yatoa onyo kali kwa Marekani kwa kusogeza meli ya kivita kwao
Ray C awaka baada ya kudaiwa amekutwa kwenye chimbo la Dawa za kulevya