Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Nchini Kenya, Raila Odinga amesema kuwa hayuko tayari kushiriki katika marudio ya uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 17 mwaka huu.

Amesema kuwa anataka kuwepo kwa mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika ili kuwepo na usawa kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo  ambao ni wa marudio.

Aidha, amesema kuwa anataka Tume ya Uchaguzi nchini humo kufanyiwa mabadiliko, ambapo imelaumiwa na mahakama kuu kwa wa kuendesha uchaguzi huo uliopita kwa njia ambayo haikuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutwa kwa matokeo.

Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kuwa uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba mwaka huu ambapo ndiyo yatakayoamua mshindi wa uraisi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi nchini Kenya, Wafula Chebukati amesema kuwa uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais ambao ni, Rais Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Zamani, Raila Odinga.

India yailalamikia Tanzania kwa utapeli, Mwijage kushughulikia suala hilo.
Diane Rwigara atiwa mbaroni