Kiongozi mkuu wa muungano wa wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga ametangaza kutoshiriki katika uchaguzi mkuu wa marudio unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Odinga amesema kuwa anataka uchaguzi ufanyike kama ilivyoamriwa na mahakama kuu nchini humo ili kuhakikisha unafanyika kwa uhuru na haki ili kuweza kuondokana na malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza.

Hata hivyo, Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama kuu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Korea Kaskazini yaiba mafaili ya jeshi la Korea Kusini - Marekani
Kocha Toto Africans azuiwa kukaa kwenye benchi