Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Omolo Odinga, akiwa kwenye mazishi ya Mbunge wa nchi hiyo Francis Nyenze eneo la Kitui amezungumza na kusema ataapishwa kuwa Rais hata kama itamgharimu hukumu ya kifo kwani lazima haki itendeke.

“Iwapo kifo ndio gharama ambayo lazima tuilipe kwa haki ya uchaguzi Kenya, na kwamba hakutakuwa na dhuluma za uchaguzi tena baadaye, tupo tayari kulipa hiyo gharama, tutaapishwa na wafanye kile wanataka kufanya”, alisikika Raila Odinga.

“Tulisema tulishinda uchaguzi na tutaapishwa, tumeonywa kwa hukumu na kifo, nataka nimwambie Githu Muigai (Mwanasheria Mkuu wa Kenya) na bosi wake, tutaapishwa na tutakufa”, amesema Odinga.

Odinga aliendelea kwa kusema kwamba alishinda uchaguzi wa Agosti 2017 ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu, na kuapa kuendelea kupambana kuleta mabadiliko katika uongozi wa nchi.

Hivi karibuni Mwanasheria MKuu wa Kenya amemuonya Raila Odinga kuendelea na mpango wake wa kujiapisha wakati tayari kuna Rais aliyeapishwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, na kusema kwamba sheria itachukua mkondo wake.

 

 

JPM atoa onyo kali kwa wanaofoji takwimu
LIVE: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi jengo la ofisi ya Takwimu