Nairobi Kenya, Mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani (NASA), Raila Odinga amewataka wafuasi wake kujizuia kufanya ngono siku ya uchaguzi mkuu Agosti, 8 mwaka huu.
Raila aliwaambia wafuasi wake kufanya ngono siku hiyo utakuwa ni mkosi hivyo aliwataka kujizuia kushiriki tendo hilo.
”Mnapokwenda vitani, ngono ni mkosi,” amesema Raila Odinga .
Kwa mujibu wa vyombo vya habari Kenya, Odinga alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita alipofanya kampeni katika maeneo ya Cheptais, Sirisia na Bumula wilayani Bungoma.
-
Hakuna fisadi wala mla rushwa atakayepona awamu hii-Lubinga
-
Mwigulu ang’aka, atishia kuzifuta taasisi zinazotetea mimba na ushoga
Raila ameongeza kwa kusema muungano wao utakuwa unahesabu kura na kutangaza matokeo.
”Tutakuwa waangalifu katika vituo vyote vya kupigia kura, tutahesabu kura zetu na kutangaza matokeo yetu na tutalinganisha na yale yaliyoko IEBC,” amesema Odinga.