Ni utaratibu wa tangu enzi o1kuwa kipindi cha msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya watu hueneza upendo na furaha baina yao.
Suala hili hupendeza zaidi pale viongozi na watu mashuhuri kutoka nyanja tofauti wanapotumia nafasi zao kama mifano ya kuigwa katika jamaii.
Hilo limetazamwa na kuzingatiwa na kiongozi wa chama maarufu nchini Kenya cha Orange Democratic Movementi ‘ODM’ Raila Odinga ambaye ameamua kujitolea misaada kwa watoto katika nyumba tofauti za kulelea watoto wenye uhitaji
Waziri mkuu huyo wa zamani wa Kenya amewavutia maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha kadhaa zikimuonyesha akiwa katika hafla hiyo fupi akigawa zawadi kwa watoto huku akiwa amevalia mavazi ya father Christmas
Katika hotuba fupi aliyoitoa, Odinga aliwatakia watoto Krismasi njema na mwaka Mpya wa 2022 wenye mafanikio, na kuwataka wawe waangalifu katika kipindi hiki cha sikukuu ili kuepuka kuambukizwa Covid-19.
Odinga pamoja na Gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o pia waliwafurahisha watoto kwa nyimbo na ngoma zao wakati wa hafla hiyo ya kuelekea sherehe za siku kuu ya Krismas.