Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesema kuwa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo hayawezi kuepukika kwa namna yoyote ile na kwamba hata walio madarakani hawawezi kuzuia kura ya maoni kuhusu katiba.

Amesema kuwa hakuna katiba iliyo kamilika duniani kote lakini ipo haja ya kuibadili katiba ya Kenya ili kupunguza ugumu wa maisha kwa raia, kwani imedhihirika kwamba ina makosa.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wafuasi wake katika Kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya, ambapo amesema kuwa muda wa kubadilisha Katiba ya Kenya umewadia.

Aidha, Odinga amesema kuwa kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni jinsi ya kuwaunganisha Wakenya wote baada ya mkutano kati yake na Uhuru Kenyatta.

“Tuna katiba mpya ndio. lakini kama ilivyo kwa Katiba zingine kote dunaini, zinahitaji kufanyiwa majaribio baada ya miaka nane ili kujua kilicho sawa na kile ambacho si sawa kwa watu wetu. hii ndio sababu tunataka mabadiliko ya katiba na hakuna anayeweza kuzuia wazo ambalo mda wake umefika. mda wa kubadilisha katiba yetu ni sasa na kama hutaki, jiondoe. tutakutana uwanjani,” amesema Odinga

Waliohukumiwa kifungo cha maisha watoroka, Serikali yawasaka kwa udi na uvumba
Video: Dodoma yaibuka kidedea, Mbeya yashika mkia ukusanyaji mapato