Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesema kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu wa kuidhinisha uchaguzi wa marudio ni batili na kwamba hawautambui.

Katika taarifa iliyotolewa na gazeti la daily Nation,imesema kuwa Odinga kupitia taarifa iliotolewa na mshauri wake Salim Lone, amesema kuwa serikali ya Jubilee sio halali akiongeza kuwa uamuzi huo wa mahakama ya juu ulifanywa kwa shinikizo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta.

”Sisi watu wa Nasa tayari, tulikuwa tumeamua kabla ya uamuzi wa mahakama kwamba hatuitambui serikali ya Uhuru Kenyatta, uamuzi huo haujabadilishwa na uamuzi wa mahakama ya juu ambao haukutushangaza. ni uamuzi uliotolewa chini ya shinikizo kubwa, hatushutumu mahakama tunaihurumia kwa kupewa shinikizo na Rais Kenyatta,”amesema Lone

Hata hivyo, kulingana na gazeti hilo, Lone amedai kwamba mahakama ilikutana chini ya shinikizo kubwa, baada ya kushindwa kukutana kutokana na wasiwasi mkubwa wa kiusalama kufuatia kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa dereva wa naibu jaji mkuu kabla ya kusikilizwa kwa kesi ya uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba.

Serikali kuvifunga vyuo vya afya visivyokidhi vigezo
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 21, 2017