Wapiga kura nchini Kenya wanaendelea na zoezi la upigaji kura kumchagua rais baada ya uchaguzi wa awali uliompa ushindi, Uhuru Kenyatta kubatilishwa na mahakama ya juu lakini upinzani bado wanaendelea kususia uchaguzi huo.

Katika hotuba yake kwa taifa  hapo jana Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upigaji kura huku akiwahakikishia usalama wa kutosha.

Amesema kuwa kila Mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote, pia ametoa tahadhari na onyo Kwa yeyote mwenye mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali itamshughulikia ipasavyo.

Hata hivyo, kwa upande wake kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani NASA, Raila Odinga amesisitiza kuwa hatashiriki uchaguzi wa leo. huku akiwataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo huku akiuita ni shughuli za maonyesho ya Jubilee.

 

Video: Giza nene uchaguzi Kenya, Polisi kikaangoni
Samatta amaliza ukame wa mabao